Gundua programu hizi za Biblia wakati wa Mwezi wa Kimataifa wa Biblia…

Sherehekea Mwezi wa Biblia Duniani

Je, ulijua kwamba YouVersion ina Familia ya Programu za Biblia? Kutoka kwa watoto, hadi vijana, hadi watu wazima—kila mtu hujihusisha na Neno la Mungu kwa njia tofauti. Ndiyo maana tumeunda programu zinazolenga watu wa makundi na maeneo mbalimbali.

Gundua ni programu ipi ya Biblia inayokufaa zaidi!

Tunakuletea: Bible Loop

Bible Loop ni mwanachama mpya zaidi wa Familia yetu ya Programu! Ikiwa imeundwa kwa ajili ya vijana, Bible Loop hutoa shughuli za kuvutia, vipengele shirikishi, na michezo ya kukariri na kukumbuka Maandiko. Ikiwa wewe ni kijana, au unaye kijana maishani mwako, hutataka kukosa hii.

App Store | Google Play

Apu ya Biblia ya Watoto

Programu hii ni kwa ajili ya watoto wadogo walio maishani mwako. Katika Bible App for Kids, utagundua hadithi za Biblia zinazovutia na michezo shirikishi iliyoundwa kuwasaidia watoto kuipenda Mungu na Neno Lake.

App Store | Google Play

Apu ya Biblia

Kutana na programu ya Biblia iliyopakuliwa zaidi duniani! Ukiwa na ufikiaji wa zaidi ya tafsiri 3,500, lugha 2,300, na maelfu ya Mipango ya Biblia, haijawahi kuwa rahisi hivi kutumia muda katika Neno la Mungu kwa njia inayokufaa.

App Store | Google Play

Biblia App Lite

Bible App Lite hukuwezesha kulipata Neno la Mungu bila intaneti, mahali popote, wakati wowote. Programu hii inapatikana katika maeneo teule.

Google Play

Shiriki Changamoto ya Siku 30 kwa kupakua mojawapo ya programu hizi! Na, kuanzia Novemba 1, jihusishe na Bible App kwa siku 30 mfululizo, na upate Beji maalum ya Mwezi wa Kimataifa wa Biblia.

Jiunge Sasa

Share this post:

Chapisho hili linapatikana pia katika: Kiingereza Kiafrikana Kiindoneshia Kijerumani Kihispania Kifilipino (Kitagalogi) Kifaransa Kitaliano Kiholanzi Kireno Kiromania Kirusi Kijapani Luga ya China (Rahisishwa) Luga ya China (Kihasili) Kikorea Kiarabu Kibelarusi Kibangali Kibulgaria Kideni Kifini Kigiriki Kiebrania Kihindi Kihangaria Kimalayi Kimongolia Kinepali Kinorwiji Kipoli Kireno (Ureno) Kislovaki Kiswedi Kitamili Kithai Kiukreni Kiurdu Kivietinamu Kizulu Kicheki Kikhmer Kimalei Kihispania (Uhispania) Kilithuania Kimasedonia Barma ya Myanmar (Zawgyi) Mserbia Armenian Kiaislandi Kikroeshia Kialbania Kiweli Kikatalani Kilatvia Kikreoli cha Haiti Kishona Inakuja hivi karibuni Kixhosa Kiyoruba