Mipango ya usomaji – Novemba 2022

Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini

Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini

25  
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

26  
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

27  
Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

28  
Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

29  
nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

30  
Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

31  
Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

32  
Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

33  
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

34  
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Matthew 6 in Swahili

Matthew 6 in English

Mipango ya usomaji – Oktoba 2022

Mipango ya usomaji – Agosti 2022

Silaha zote za Mungu

Efe 6:10-18

10  
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

11  
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12  
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13  
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14  
Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani

15  
na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani

16  
zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17  
Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu

18  
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote

Ephesians 6 in Swahili

Ephesians 6 in English