Zab 23: BWANA ndiye mchungaji wangu

1  
BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

2  
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3  
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4  
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5  
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.

6  
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Psalm 23 in Swahili

Psalm 23 in English

BibleProject: Mihtasari ya Vitabu: Agano Jipya: Warumi

BibleProject: Mihtasari ya Vitabu - Agano Jipya

Tafakari umbo na mada msingi za kila kitabu cha Biblia kupitia maelezo ya mfano.

Muhtasari: Warumi 1-4

Muhtasari: Warumi 5-16

Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate

Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate

Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Mk 10:21-22

Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.

Mk 8:34-35

Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

Mt 10:38

Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Gal 2:20

Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?

Lk 9:23-25

akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [ Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.

Lk 22:42-43

Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

Gal 5:24

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Mt 16:24-27

Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.

Rum 8:18

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Yak 1:12

BibleProject: Mihtasari ya Vitabu: Agano Jipya: Luka – Matendo

BibleProject: Mihtasari ya Vitabu - Agano Jipya

Tafakari umbo na mada msingi za kila kitabu cha Biblia kupitia maelezo ya mfano.

Muhtasari: Luka 1-9

Muhtasari: Luka 10-24

Muhtasari: Matendo 1-12

Zaburi 91 – Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu

1  
Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2  
Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

3  
Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

4  
Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5  
Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana

6  
Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri

7  
Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8  
Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9  
Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10  
Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11  
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12  
Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13  
Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

14  
Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15  
Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza

16  
Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.