Zab 23: BWANA ndiye mchungaji wangu

1  
BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

2  
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3  
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4  
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5  
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.

6  
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Psalm 23 in Swahili

Psalm 23 in English – NKJV