Posted on 2023-02-02Mipango ya usomaji – Februari 2023 Yesu Ananipenda siku 7 Ikiwa mtu angekuuliza, “Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?” ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, “Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu. Ingia katika Kusudi siku 5 Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii. Muda wa kupumua siku 5 Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa… Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo. Kukombolewa kwa ndoto siku 7 Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.
Posted on 2023-01-02Mipango ya usomaji – Januari 2023 Mwaka Mpya, Rehema Mpya siku 15 Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku. Neno Moja Litakalobadilisha Maisha Yako siku 4 NENO MOJA husaidia kurahisisha maisha yako kwa kulenga tu NENO MOJA kwa mwaka mzima. Urahisishaji wa kugundua neno ambalo Mungu amekuwekea inafanya kuwa kichochezi cha maisha yako kubadilika. Vurugu na utata husababisha kuchelewesha na kulemaza, ilhali urahisishaji na lengo husababisha mafanikio na uwazi. Ibada hii ya siku nne inakuonyesha jinsi ya kupata kiini cha nia yako kwa maono ya neno moja kwa mwaka.
Posted on 2022-12-02Mipango ya usomaji – Desemba 2022 Tusome Biblia Pamoja ( Desemba) siku 31 Sehemu ya 12 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unaziongoza jamii kupitia Biblia youte pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 12 inavijumuisha vitabu vya Isaya, Mika, Petro wa Kwanza, Petro wa Pili, Yohana wa Kwanza, Yohana wa Pili, Yohana wa Tatu, Yohana na Yuda Luka siku 12 Mpango huu rahisi utakuongoza ndani ya kitabu cha Injili iliyo andikwa na Marko kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Posted on 2022-10-27Mipango ya usomaji – Novemba 2022 Tuisome Biblia Pamoja (November) siku 30 Sehemu 11 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unazielekeza jamii kupitia Biblia nzima katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 11 inajumuisha vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Ezekieli, Hosea na Ufunuo wa Yohana.
Posted on 2022-09-26Mipango ya usomaji – Oktoba 2022 Tusome Biblia Pamoja ( Octoba) siku 31 Sehemu ya 10 kati ya mfululizo wenye sehemu 12 katika mpango huu unaziongoza jamii kuipitia Biblia nzima katika siku 365. Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 10 inavihusisha vitabu vya Mhubiri, Yona, Yeremia na Maombolezi Zaburi siku 31 Usomaji wa kitabu cha Zaburi niya muhimu kwa kila muda ya haja. Wakati unapitia wakati mgumu, kitabu cha Zaburi kinaweza kua kama faraja na kuweka moyo. Naweza Kweli Kushinda Dhambi na Majaribu? siku 5 Umewahi kujiuliza, “Mbona bado napambana na dhambi hiyo?” Hata mtume Paulo alisema hivyo katika Warumi 7:15: “ Sifanyi ninachotaka, lakini nafanya kile ninachochukia.” Je, tunazuiaje dhambi kusimamisha maisha yetu ya kiroho? Je, hata inawezekana? Hebu tujadili dhambi, majaribu, Shetani, na, kwa shukrani, upendo wa Mungu. Kurejesha Furaha Yako siku 5 Ikiwa unataka furaha katika maisha yako, unapaswa kupata usawa katika ratiba yako. Mchungaji Rick anashiriki jinsi unavyoweza kurekebisha mchango wako na matokeo yako ili kutoa na kupokea kwako kukusaidia kurejesha furaha yako, si kuipoteza.