Posted on Juni 25, 2023Mipango ya usomaji – Julai 2023 Ngumu na Lisa Bevere siku 6 Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura. Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku – Hekima siku 5 Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, “Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako.”Biblia inasema, “Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.” Zaburi 119:2 (BHN) Adui wa Moyo siku 5 Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adui wanne wa moyo — hatia, hasira, tamaa, na wivu — na kukufunza jinsi ya kuwaondoa. Share this post:
Posted on Aprili 28, 2023Mipango ya usomaji – Mei 2023 Kugeuka na Kurudi Upande wa Pili Kutoka Uraibu siku 3 Ikiwa maisha yako hayako katika mpangilio na Neno la Mungu, hakika utapatwa na matokeo machungu. Wengi wamepambana na afya yao, kupoteza ajira, na mahusiano, na kujipata kwamba wanahisi kwamba wapo mbali na Mungu kwa sababu ya uraibu. Inaweza kuwa uraibu wenye uzito kama vile mihadarati au ponografia ama uraibu ndogo, kama chakula ama burudani, uraibu unavuruga maisha yetu. Mruhusu mwandishi mashuhuri Tony Evans akuonyesha njia ya uhuru. Mbona Mungu ananipenda? siku 5 Maswali: Ikija kwa Mungu, tuna maswali mengi sana. Kwa sababu ya tamaduni zetu, swali moja ambalo tutajipata tukijiuliza ni, “Mbona Mungu ananipenda?” au “Ni vipi atanipenda?” Mpango huu unashirikisha jumla ya vifungu 26 vya Biblia—Kila kifungu kikiongea juu ya upendo wa Mungu usiokuwa na shaka. Share this post:
Posted on Machi 30, 2023Mipango ya usomaji – Aprili 2023 Kwa nini Pasaka? siku 5 Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke kujua haya? Katika mpango huu wa siku tano, Nicky Gumbel anatoa majibu ya kuvutia kwa maswali hayo. 1 & 2 Timotheo siku 5 Mpango huu ita kuchukua ndani ya 1 & 2 Timotheo na itakua vizuri kwa usomaji wa upekee ama ya kundi. Share this post:
Posted on Machi 2, 2023Mipango ya usomaji – Machi 2023 Siku Sita Za Majina Ya Mungu siku 6 Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God’s Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017. Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila Siku siku 7 Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog. Ipe Kazi Yako Maana siku 4 Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John Piper siku 7 Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu Share this post:
Posted on Febuari 2, 2023Mipango ya usomaji – Februari 2023 Yesu Ananipenda siku 7 Ikiwa mtu angekuuliza, “Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?” ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, “Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu. Ingia katika Kusudi siku 5 Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii. Muda wa kupumua siku 5 Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa… Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo. Kukombolewa kwa ndoto siku 7 Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena. Share this post: