Posted on 2020-01-012021-10-01Mipango ya usomaji – Januari 2020 Tabia siku 6 Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu. Mwaka Mpya, Rehema Mpya siku 15 Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku. Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa Yesu siku 7 Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia. “Nenda Tenda Sema Toa” ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu. Siku 21 za Kufunga siku 21 Anza mwaka mpya kwa kulenga nidhamu ya kiroho ya kufunga. Mpango huu unajumuisha vifungu kadhaa kuhusu kufunga, vingine vinahimiza kutafakari ukaribu na Mungu. Kwa siku 21, utapata somo la Biblia la kila siku, ibada fupi, maswali ya kutafakari, na maombi.