|
|
|
Mipango ya usomaji – Septemba 2020
Mipango ya usomaji – Agosti 2020
Mipango ya usomaji – Julai 2020
Upendo huvumilia, hufadhili
4
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni
5
haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya
6
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli
7
huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8
Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
9
Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu
10
lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.
11
Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
12
Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
13
Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.