Upendo huvumilia, hufadhili

Upendo huvumilia, hufadhili

4  
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni

5  
haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya

6  
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli

7  
huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8  
Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

9  
Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu

10  
lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.

11  
Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

12  
Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

13  
Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

1 Corinthians 13 in Swahili

1 Corinthians 13 in English

Chapisho hili linapatikana pia katika: Kireno Kiarabu Kibelarusi Kibangali Kibulgaria Kideni Kifini Kijojia Kigiriki Kihindi Kihangaria Kimalayi Kimongolia Kinepali Kinorwiji Kireno (Ureno) Kisinhala Kislovaki Kiswedi Kitamili Kitelugu Kituruki Kizulu Kicheki Kimalei Kihispania (Uhispania) Kilithuania Marathi Kipunjabi Kigujarati Kimasedonia Kiamhariki Kiuzbeki