Posted on 2021-03-312021-06-08Mipango ya usomaji – Machi 2021 MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama Mkristo Siku 5 Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema! Mwongozo wa KiMungu Siku 7 Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia. Vitendo vya Toba Siku 5 Toba ni moja ya hatua muhimu sote huchukua tunapokuja kumjua Yesu kristo kama mwongozi wa maisha yetu. Toba ni kitendo chetu na msamaha ni majibu ya Mungu kwetu kutokana na mapenzi yake kamili kwa ajili yetu. Ndani ya siku tano na kupitia masomo haya, utapokea somo la biblia kila siku na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kuelewa vyema umuhimu wa toba katika kutembea kwetu na Kristo.
Posted on 2021-03-152021-06-15Mistari maarufu ya Biblia – Machi 2021 – Ikiwa watu wangu… Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. 2 Tim 1:7 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 2 Nya 7:13-14 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Isa 41:10 Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita. Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa. Isa 26:20-21 Najikumbusha neno hili,Kwa hiyo nina matumaini.Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,Kwa kuwa rehema zake hazikomi.Ni mpya kila siku asubuhi;Uaminifu wako ni mkuu.BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,Kwa hiyo nitamtumaini yeye. Omb 3:21-24 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Yak 1:12 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. Ebr 13:16 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juuAtakaa katika uvuli wake Mwenyezi.Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini. Zab 91:1-2
Posted on 2021-03-012021-10-15Mipango ya usomaji – Machi 2021 Kutafuta Amani siku 10 Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu–Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo. Kufuata Amani siku 7 Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano yako na wengine na uombee dunia tunayoishi. Somo hili linatumia hekima kutoka methali za Afrika kutusaidia kufunua amani ya kweli ya Mungu. Amani ya Mungu siku 4 Neno la Mungu linatuambia kwamba Hutoa amani ” ipitayo ufahamu wote” (Wafilipi 4:7 SUV). Katika mafundisho haya ya siku nne, wewe na watoto wako muamgalie kwa makini maeneo katika maisha yetu tunapoweza kupata amani hiyo. Kila siku inajumuisha hitaji la maombi, kusoma maandiko kidogo na ufafanuzi, mazoezi ya kufanya, na maswali ya kujadili. Oswald Chambers: Amani – Maisha kwenye Roho siku 30 Amani: Maisha ya Roho ni hazina ya msukumo ya nukuu kutoka kwenye kazi za Oswald Chambers, mwandishi mpendwa ulimwenguni wa ibada na mwandishi wa My Utmost for His Highest. Pata mapumziko kwa Mungu na pata uelewa zaidi wa umuhimu wa amani ya Mungu kwenye maisha yako. Waebrania wiki 1 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Waebrania na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Tumaini Linaloishi: Hesabu kuelekea Pasaka siku 3 Giza linapokuzunguka, ulikabili namna gani? Kwa siku 3 zijazo, zama katika hadithi ya Pasaka na ugundue jinsi ya kushikilia tumaini pale unapojisikia kuachwa, mpweke au usiye wa thamani.
Posted on 2021-02-012021-10-15Mipango ya usomaji – Februari 2021 Mwongozo wa KiMungu siku 7 Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia. Maombi siku 21 Kujifunza namns ya kuomba vizuri, kutoka kwa maombi ya mwaminifi pia na maneno ya Yesu Mwenyewe. Kupata faraja ya kuendelea kuomba Mungu kila siku, pamoja na kudumu na uvumilivu. Chunguza mifano tupu, maombi ya uhaki wa mwenyewe, ikipimwa na maombi ya kweli ya walio na moyo safi. Omba bila kuacha. Maombi Hatari siku 7 Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, “Dangerous Prayers” yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.
Posted on 2021-01-312021-06-07Mipango ya usomaji – Januari 2021 Vitendo vya Toba Siku 5 Toba ni moja ya hatua muhimu sote huchukua tunapokuja kumjua Yesu kristo kama mwongozi wa maisha yetu. Toba ni kitendo chetu na msamaha ni majibu ya Mungu kwetu kutokana na mapenzi yake kamili kwa ajili yetu. Ndani ya siku tano na kupitia masomo haya, utapokea somo la biblia kila siku na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kuelewa vyema umuhimu wa toba katika kutembea kwetu na Kristo. Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi! Siku 7 Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt Maombi Siku 21 Kujifunza namns ya kuomba vizuri, kutoka kwa maombi ya mwaminifi pia na maneno ya Yesu Mwenyewe. Kupata faraja ya kuendelea kuomba Mungu kila siku, pamoja na kudumu na uvumilivu. Chunguza mifano tupu, maombi ya uhaki wa mwenyewe, ikipimwa na maombi ya kweli ya walio na moyo safi. Omba bila kuacha. Mwongozo wa KiMungu Siku 7 Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia. Mpango Bora wa Kusoma Siku 28 unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia. Wasiwasi Siku 7 Maisha yetu unaweza kwa urahisi hivyo kuwa kuzidiwa na wasiwasi na hofu ya haijulikani. Lakini Mungu ametupa Roho wa ujasiri, si ya hofu na wasiwasi. Mpango huu siku saba itasaidia kurejea kwa Mungu katika kila hali. Mwisho mwisho kwa wasiwasi ni kuweka imani yako katika Mungu. Tabia SIku 6 Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.