Posted on 2023-12-01Mipango ya usomaji – Desemba 2023 Luka siku 12 Mpango huu rahisi utakuongoza ndani ya kitabu cha Injili iliyo andikwa na Marko kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Tusome Biblia Pamoja ( Desemba) siku 31 Sehemu ya 12 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unaziongoza jamii kupitia Biblia youte pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 12 inavijumuisha vitabu vya Isaya, Mika, Petro wa Kwanza, Petro wa Pili, Yohana wa Kwanza, Yohana wa Pili, Yohana wa Tatu, Yohana na Yuda
Posted on 2023-11-01Mipango ya usomaji – Novemba 2023 Tuisome Biblia Pamoja (November) siku 30 Sehemu 11 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unazielekeza jamii kupitia Biblia nzima katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 11 inajumuisha vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Ezekieli, Hosea na Ufunuo wa Yohana. Wagalatia siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Wagalatia na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.
Posted on 2023-09-02Mipango ya usomaji – Septemba 2023 Tusome Biblia Pamoja (Septemba) siku 30 Sehemu ya 9 kati ya 12 kwenye mpangilio unaoongoza jamii kusoma Biblia nzima pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 9 inajuisha vitabu vya Nehemia, Esta, Timotheo wa kwanza na wa pili, Yoeli, Amosi, Obadia, Nahumu, Habakuki, Sefania, Tito, Philomeno, Yakobo, Hagai Zekarai na Malaki
Posted on 2023-06-25Mipango ya usomaji – Julai 2023 Ngumu na Lisa Bevere siku 6 Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura. Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku – Hekima siku 5 Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, “Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako.”Biblia inasema, “Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.” Zaburi 119:2 (BHN) Adui wa Moyo siku 5 Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adui wanne wa moyo — hatia, hasira, tamaa, na wivu — na kukufunza jinsi ya kuwaondoa.
Posted on 2023-04-28Mipango ya usomaji – Mei 2023 Kugeuka na Kurudi Upande wa Pili Kutoka Uraibu siku 3 Ikiwa maisha yako hayako katika mpangilio na Neno la Mungu, hakika utapatwa na matokeo machungu. Wengi wamepambana na afya yao, kupoteza ajira, na mahusiano, na kujipata kwamba wanahisi kwamba wapo mbali na Mungu kwa sababu ya uraibu. Inaweza kuwa uraibu wenye uzito kama vile mihadarati au ponografia ama uraibu ndogo, kama chakula ama burudani, uraibu unavuruga maisha yetu. Mruhusu mwandishi mashuhuri Tony Evans akuonyesha njia ya uhuru. Mbona Mungu ananipenda? siku 5 Maswali: Ikija kwa Mungu, tuna maswali mengi sana. Kwa sababu ya tamaduni zetu, swali moja ambalo tutajipata tukijiuliza ni, “Mbona Mungu ananipenda?” au “Ni vipi atanipenda?” Mpango huu unashirikisha jumla ya vifungu 26 vya Biblia—Kila kifungu kikiongea juu ya upendo wa Mungu usiokuwa na shaka.