Wakati tumaini lilipoonekana kutokuwepo, Mungu alikutana na Alice.

Tahadhari kuhusu maudhui: hadithi ifuatayo ina mada za kujidhuru na huzuni ambazo zinaweza kuwaumiza baadhi ya wasomaji.

Wakati tumaini lilipoonekana kutokuwepo, Mungu alikutana na Alice.

Alice alipokuwa na miaka kumi na sita, alihisi amenaswa na maumivu na hasara, akiwa amelemewa na huzuni na upweke.

Hali ya kukata tamaa ilipozidi, usiku mmoja aliamua kujiua. Na hapo ndipo jambo lisiloelezeka lilipotokea.

Akiwa juu ukingoni mwa ghorofa yake, upepo mkali wa ghafla ulimfanya aanguke nyuma ndani ya chumba chake badala ya mbele.

Akiwa amelala chini, akiwa ameshtuka na akilia, Alice alipokea ujumbe kutoka kwa jirani yake akimwalika kanisani. Alikubali kwenda, na hapo ndipo alipogundua kwa mara ya kwanza Programu ya Biblia.

Wakati tumaini lilipoonekana kutokuwepo, Mungu alikutana na Alice.

Alianza Mpango wa Biblia na kupitia huo, alipata tumaini na akamkabidhi Yesu maisha yake.

Leo, Alice anaunda na kuchapisha Mipango ya Biblia akiwa Mshirika wa YouVersion kupitia programu ileile iliyomtambulisha kwa Yesu. Hajajaa matumaini tu — anayasambaza.

Je, unamjua mtu katika maisha yako anayemhitaji Mungu kwa dhati? Mtambulishe kwenye Programu ya Biblia, na umwombe Mungu amjaze tumaini.

Share this post:

Chapisho hili linapatikana pia katika: Kiingereza Kiafrikana Kiindoneshia Kijerumani Kihispania Kifilipino (Kitagalogi) Kifaransa Kitaliano Kiholanzi Kireno Kiromania Kirusi Kijapani Luga ya China (Rahisishwa) Luga ya China (Kihasili) Kikorea Kiarabu Kibelarusi Kibangali Kibulgaria Kideni Kifini Kigiriki Kiebrania Kihindi Kihangaria Kimalayi Kimongolia Kinepali Kinorwiji Kifarsi Kipoli Kireno (Ureno) Kislovaki Kiswedi Kitamili Kitelugu Kithai Kituruki Kiukreni Kiurdu Kivietinamu Kizulu Kicheki Kikhmer Kimalei Barma ya Myanmar (Unicode) Kilithuania Kimasedonia Barma ya Myanmar (Zawgyi) Mserbia Armenian Kiaislandi Kikroeshia Kialbania Kiweli Kikatalani Kilatvia Kikreoli cha Haiti Kishona Inakuja hivi karibuni Kixhosa Kiyoruba Igbo Serbian (Latin) Slovenian