Posted on 2022-01-27Mipango ya usomaji – Februari 2022 Tusome Biblia Pamoja (Februari) siku 28 Sehemu ya 2 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia nzima pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikizi—sikiliza chini ya dakika 20 kila siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka kwa Agano Jipya na Agano la Kale, na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya Pili inajumuisha vitabu vya Mwanzo, Kutoka, Walawi na Wagalatia. Marko siku 8 Mangu huu rahisi utakuongoza ndani ya kitabu cha Injili iliyo andikwa na Marko kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Posted on 2022-01-02Mipango ya usomaji – Januari 2022 Tusome Biblia Pamoja (Januari) siku 31 Sehemu ya kwanza ya msururu wa sehemu 12, mpango huu huongoza jamii kupitia Biblia yote pamoja kwa siku 365. Waalike wengine kujiunga kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na la Kale, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote kote. Sehemu ya kwanza inajumuisha vitabu vya Luka, Matendo, Danieli na Mwanzo. Yohana siku 10 Mpango huu rahisi utakuongoza kupitia njia ya Injili kulingana na Yohana kuanzia mwanzo hadi mwisho Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika Bwana siku 30 Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa “My Utmost for His Highest”, katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
Posted on 2021-12-072021-12-08Mipango ya usomaji – Desemba 2021 Yote ni Utulivu: Kupokea Pumziko la Yesu Krismasi hii siku 5 ‘Huu ni msimu wa furaha, lakini pia hakuna muda. Jitenge kwa muda mfupi ya mapumziko na ibada ambao utakulisha unapofanya kazi ya furaha msimu huu. Mpango huu wa siku tano umetoka kitabu Kufungua Majina ya Yesu: Mafunzo kutoka Biblia kuhusu Ujio (Unwrapping the Names of Jesus: An Advent Devotional) na utakuongoza kupokea pumziko la Yesu Krismasi huu kwa kuchukua muda kukumbuka wema wake, kudhihirisha uhitaji wako, kutafuta utulivu wake, na kutumainia uaminifu wake. Tumaini la Krismasi siku 10 Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehekea Krismasi na kwa nini inafaa ibadilishe sio tu vile unasherehekea sikukuu hiyo lakini pia maisha yako kwa ujumla.
Posted on 2021-11-012021-10-28Mipango ya usomaji – Novemba 2021 1 & 2 Petro siku 4 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha 1 & 2 Petro na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Tuisome Biblia Pamoja (November) siku 30 Sehemu 11 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unazielekeza jamii kupitia Biblia nzima katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 11 inajumuisha vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Ezekieli, Hosea na Ufunuo wa Yohana. Vitendo vya Toba siku 5 Toba ni moja ya hatua muhimu sote huchukua tunapokuja kumjua Yesu kristo kama mwongozi wa maisha yetu. Toba ni kitendo chetu na msamaha ni majibu ya Mungu kwetu kutokana na mapenzi yake kamili kwa ajili yetu. Ndani ya siku tano na kupitia masomo haya, utapokea somo la biblia kila siku na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kuelewa vyema umuhimu wa toba katika kutembea kwetu na Kristo.
Posted on 2021-10-012021-09-22Mipango ya usomaji – Oktoba 2021 Yakobo Siku 3 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Yakobo na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja ( Octoba) Siku 31 Sehemu ya 10 kati ya mfululizo wenye sehemu 12 katika mpango huu unaziongoza jamii kuipitia Biblia nzima katika siku 365. Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 10 inavihusisha vitabu vya Mhubiri, Yona, Yeremia na Maombolezi Kuamini Mungu ni vyema Bila kujali lolote Siku 5 Kuna jumbe fulani siku hizi, nje na ndani ya Kanisa, ambazo zimepaka tope ujumbe wa kweli wa fadhili za Mungu. Ukweli ni kwamba, Mungu hashurutishwi kutupea vitu vizuri—lakini anataka! Siku tano zijazo zitakusaidia kuangalia upya kando yako kwa macho yanayoona vitu vinavyokupotosha kila siku na kuona wema chungu nzima wa Mungu.