Posted on 2021-09-052021-09-20Mipango ya usomaji – Septemba 2021 Wagalatia Siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Wagalatia na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Septemba) Siku 30 Sehemu ya 9 kati ya 12 kwenye mpangilio unaoongoza jamii kusoma Biblia nzima pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 9 inajuisha vitabu vya Nehemia, Esta, Timotheo wa kwanza na wa pili, Yoeli, Amosi, Obadia, Nahumu, Habakuki, Sefania, Tito, Philomeno, Yakobo, Hagai Zekarai na Malaki Kutumia muda wako kwa ajili ya Mungu Siku 4 Ibada ya siku nne kutoka kwa R.C. Sproul, jinsi ya kutumia wakati wako kwa ajili ya Mungu. Kila Ibada inakuhimiza kuishi katika uwepo wa Mungu, chini ya mamlaka ya Mungu, kwa utukufu wa Mungu.
Posted on 2021-08-05Mipango ya usomaji – Agosti 2021 Waefeso Siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Waefeso na ni cha maana kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Agosti) Siku 31 Sehemu ya 8 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia nzima pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikizi—sikiliza chini ya dakika 20 kila siku. Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na Agano la Kale, na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya 8 inajumuisha kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Kwanza na ya Pili, Wathesalonike wa kwanza na Pili na Ezra. Mazungumzo na Mungu Siku 12 Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote – mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda! Mpango wa kupigana Vita vya Kiroho Siku 5 Kwa haya mafundisho ya nguvu utaelewa kwa kina kuhusu jinsi ya kutengeneza njia ya kumpita adui na kuzuia mpango wake wa kuharibu maisha yako
Posted on 2021-07-102021-07-26Mipango ya usomaji – Julai 2021 1 Wakorintho Siku 8 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha 1 Wakorintho na itakua ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Julai) Siku 31 Sehemu ya 7 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia yote pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge nawe kila wakati unapoaza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano la Kale na Agano Jipya, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote kote. Sehemu ya saba inajumuisha vitabu vya Samueli wa Pili, Wafalme wa Kwanza na wa Pili na Mariko. Mbona Mungu ananipenda? Siku 5 Maswali: Ikija kwa Mungu, tuna maswali mengi sana. Kwa sababu ya tamaduni zetu, swali moja ambalo tutajipata tukijiuliza ni, “Mbona Mungu ananipenda?” au “Ni vipi atanipenda?” Mpango huu unashirikisha jumla ya vifungu 26 vya Biblia—Kila kifungu kikiongea juu ya upendo wa Mungu usiokuwa na shaka. Kuweka Muda Wa Kupumzika siku 5 Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu.
Posted on 2021-06-302021-07-05Mipango ya usomaji – Juni 2021 Maombi Hatari Siku 7 Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, “Dangerous Prayers” yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini. Kutafuta Njia ya Kumrudia Mungu Siku 5 Je, unatafuta mengi kutoka kwa maisha? Kutaka mengi ni kuwa na hamu ya kumrudia Mungu— popote uhusiano wako na Mungu upo sasa. Sisi sote hushuhudia ishara—au muamko—tunapotafuta kumrudia Mungu. Safari kupitia kwa moja wepo ya miamko hizi na kupunguza umbali kati ya ulipo sasa na wapi unataka kuwa. Tunataka kumpata Mungu, anataka hata mengi yapatikane.. Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi! Siku 7 Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt Maombi ya Yesu Siku 5 Tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika uhusiano, na uhusiano wetu na Mungu sio tofauti. Mungu anataka tuwasiliane naye kwa maombi—Kitu ambacho hata mwanawe, Yesu Kristo alifanya. Katika mpango huu, utajifunza kutoka kwa mfano wa Yesu, na utapewa changamoto ya kutoka katika shughuli nyingi za maisha na ujionee nguvu na mwongozo maombi hutoa. Kutafuta Amani Siku 10 Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu–Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo. Kuua Nguvu zinazoangamiza na John Bevere Siku 7 Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung’oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka. 1 & 2 Timotheo Siku 5 Mpango huu ita kuchukua ndani ya 1 & 2 Timotheo na itakua vizuri kwa usomaji wa upekee ama ya kundi. Kubarikiwa Siku 7 Unaishi vipi maisha yaliyo barikiwa? Naamini kila mtu anahamu na anatafuta jibu hili. Miongoni mwa wahusika mbalimbali katika Biblia, kuna mmoja hasa ambaye napenda. Jina lake halijatajwa, lakini anaishi kwa kanuni za Biblia. Huyu shujaa wangu wa Kibiblia ndiye mtu mwema aliyetajwa katika Zaburi 112.
Posted on 2021-05-012021-10-15Mipango ya usomaji – Mei 2021 Uhakika siku 4 Uhakika wewe ni kusamehewa na Mungu ni mapenzi ya Mungu! Uhakika wako kukua kupitia kukutana na Mungu na kutafakari Neno lake. Aya zifuatazo, wakati kujikumbusha, inaweza kukusaidia mapumziko uhakika katika Mungu katika yote ya siku yako. Hebu maisha yako mgeuzwe kwa kukariri maandiko! Kwa mfumo wa kina kwa kukariri maandiko, kutembelea www.MemLok.com Warumi siku 8 Mpango huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Waroma na niya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Mei) siku 31 Sehemu ya 5 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu huongoza jamii kupitia Biblia yote kwa siku 365 pamoja. Waalike wengine kujiunga nawe kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya kazi vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kwa siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano la Kale na Agano Jipya, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya 5 inahusisha vitabu vya Wakorintho wa Kwanza na wa Pili, Kumbukumbu la Torati na Yoshua. Kutafuta Njia ya Kumrudia Mungu siku 5 Je, unatafuta mengi kutoka kwa maisha? Kutaka mengi ni kuwa na hamu ya kumrudia Mungu— popote uhusiano wako na Mungu upo sasa. Sisi sote hushuhudia ishara—au muamko—tunapotafuta kumrudia Mungu. Safari kupitia kwa moja wepo ya miamko hizi na kupunguza umbali kati ya ulipo sasa na wapi unataka kuwa. Tunataka kumpata Mungu, anataka hata mengi yapatikane..