Posted on 2020-10-012021-10-11Mipango ya usomaji – Oktoba 2020 1 & 2 Petro siku 4 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha 1 & 2 Petro na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John Piper siku 7 Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu
Posted on 2020-09-012021-10-11Mipango ya usomaji – Septemba 2020 Ipe Kazi Yako Maana siku 4 Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. Hatua Sita Ya Uongozi Bora Zaidi siku 7 U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua. Adui wa Moyo siku 5 Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adui wanne wa moyo — hatia, hasira, tamaa, na wivu — na kukufunza jinsi ya kuwaondoa. Kuua Nguvu zinazoangamiza na John Bevere siku 7 Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung’oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka.
Posted on 2020-08-012021-10-11Mipango ya usomaji – Agosti 2020 Kutafuta Amani siku 10 Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu–Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo. Kutafuta Karoti siku 7 Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani–kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti. Tumaini, Jibidishe, Na Pumzika siku 4 Biblia inatuagiza kufanya kazi kwa bidii, lakini pia inatuambia ni Mungu– siyo sisi –anayetoa matunda ya kazi yetu. Kama mpango huu wa siku nne utakavyoonesha, taaluma ya kikristo lazima ikubali mvutano kati ya “kuamini” na “kujibidisha” ili kupata mapumziko halisi ya Sabato. Waefeso siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Waefeso na ni cha maana kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.
Posted on 2020-07-012021-10-11Mipango ya usomaji – Julai 2020 Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha Yako siku 5 Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi. Kuweka Muda Wa Kupumzika siku 5 Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu. Mambo yote ni mapya siku 5 Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jinsi mwenendo wa wakristo unaweza kuonekana unapingana na tabia zetu za asili, lakini inathibitisha kwamba wa milele na bora zaidi kwa nje. Katika siku tano hizi za mpango huu wa masomo, utavumbua vitu kama: jinsi ya kushughulika na mahusiano magumu, kumwamini Mungu na heshima yako, ukisimamisha utambulisho wako katika Kristo, kuelewa kusudi la mateso na upaji wa Mungu ndani yake, na jinsi tunavyotakiwa kuwa nuru ya injili ulimwenguni. Wagalatia siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Wagalatia na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.
Posted on 2020-06-012021-10-11Mipango ya usomaji – Juni 2020 1 Wakorintho siku 8 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha 1 Wakorintho na itakua ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina Baba siku 7 Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake. Ngumu na Lisa Bevere siku 6 Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.