Posted on 2019-12-23Mistari ya Biblia ya Krismasi Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele. Mik 5:2 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Isa 7:14 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Mt 1:20-21 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yn 3:16 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Isa 9:6 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Yn 1:14 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Gal 4:4-5 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Lk 2:10-11 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Lk 2:13-14 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine. Mt 2:9-12
Posted on 2019-11-012021-10-01Mipango ya usomaji – Novemba 2019 Zaburi siku 31 Usomaji wa kitabu cha Zaburi niya muhimu kwa kila muda ya haja. Wakati unapitia wakati mgumu, kitabu cha Zaburi kinaweza kua kama faraja na kuweka moyo. Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika Bwana siku 30 Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa “My Utmost for His Highest”, katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu. Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku – Hekima siku 5 Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, “Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako.”Biblia inasema, “Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.” Zaburi 119:2 (BHN) Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila Siku siku 7 Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog.
Posted on 2019-10-012021-10-01Mipango ya usomaji – Oktoba 2019 Ufunuo siku 11 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Ufunuo na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Pumua shauku ya kiroho ndani ya ndoa yako siku 7 Ikichukuliwa kutoka kitabu chake kipya “Maisha marefu ya upendo”, Gary Thomas anaongea kuhusu madhumuni ya milele ndani ya ndoa. Jufunze viungu vya maana kwa kusaidia kubeba ndoa yako ndani ya mahusiano yakujaa na mambo mapya, ikienezwa na maisha kwa wengine.
Posted on 2019-09-012021-10-01Mipango ya usomaji – Septemba 2019 Imani siku 12 Je, kuona ni kuamini? Au kuamini ni kuona? Hayo ni maswali ya imani. Mpango huu unatoa masomo ya kina kuhusu imani—kutoka kwa hadithi za Agano la Kale kuhusu watu halisia ambao walionyesha imani jasiri katika matukio yasiowezekana kwa mafundisho ya Yesu juu ya somo. Kupitia kwa kusoma kwako, utatiwa moyo ili kudumisha uhusiano wako na Mungu na uwe mfuasi mwenye imani zaidi wa Yesu. 2 Wakorintho wiki 1 Mpango huu rahisi uta kuchukua ndani ya kitabu cha 2 Wakorintho na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Muda wa kupumua siku 5 Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa… Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.
Posted on 2019-08-012021-10-01Mipango ya usomaji – Agosti 2019 1 Wakorintho siku 8 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha 1 Wakorintho na itakua ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Oswald Chambers: Amani – Maisha kwenye Roho siku 30 Amani: Maisha ya Roho ni hazina ya msukumo ya nukuu kutoka kwenye kazi za Oswald Chambers, mwandishi mpendwa ulimwenguni wa ibada na mwandishi wa My Utmost for His Highest. Pata mapumziko kwa Mungu na pata uelewa zaidi wa umuhimu wa amani ya Mungu kwenye maisha yako.