|
|
|
Mipango ya usomaji – Novemba 2022
Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini
25
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27
Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28
Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29
nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30
Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31
Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32
Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Mipango ya usomaji – Oktoba 2022
Gundua programu nyepesi ya Biblia ya nje ya mtandao kutoka kwa YouVersion!
Tayari kwenye zaidi ya vifaa milioni 2.7, programu hii mpya inakupa ufikiaji kamili wa nje ya mtandao kwa vipengele muhimu vya Bible App—yote huku ukifanya nafasi ya kuhifadhi simu yako kuwa nyepesi.
Soma Biblia nje ya mtandao, pata Sala za Kila Siku, shiriki mistari ya Biblia, sikiliza sauti za Biblia, na mengine mengi.
Endelea kushikamana na Mungu kupitia Neno Lake wakati wowote, mahali popote!
Iwapo unatafuta programu ya Biblia ya kila mtu-moja iliyo nje ya mtandao, matoleo tofauti na sauti—usitafute kwingine.
~ Davor, Nigeria
Helpful links:
YouVersion Biblia Takatifu Lite (na África)
Apu ya Biblia ya Watoto