|
||
|
||
|
||
|
||
|
||
|
||
|
||
|
Zaburi 91 – Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu
1
Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2
Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3
Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
4
Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5
Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana
6
Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri
7
Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.
8
Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9
Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
10
Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.
12
Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13
Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
14
Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15
Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza
16
Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
BibleProject: Mihtasari ya Vitabu: Agano Jipya: Mathayo – Yohana
Tafakari umbo na mada msingi za kila kitabu cha Biblia kupitia maelezo ya mfano.
|
|
|
|
|
|
|
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu
Pata programu ya bure ya Bibilia
Ni ngumu kukaa ukizingatia Mungu na Neno Lake. Ndio maana app ya bure ya Bibilia ya YouVersion inakupa nyenzo za kutafuta moyo wa Mungu kila siku: sikiliza biblia za sauti, tayarisha Maombi, Jifunze na Marafiki, chunguza matoleo ya Bibilia 2,000, na mengine zaidi. Sasa iko kwenye vifaa zaidi ya milioni 400 ulimwenguni!
Matoleo zaidi ya 2000 ya Biblia:
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Biblia Habari Njema
Neno: Bibilia Takatifu 2014
Swahili Revised Union Version
Biblia Habari Njema
Biblia Sikizi:
Biblia ya Sauti: Biblia Habari Njema
Biblia ya Sauti: Neno: Bibilia Takatifu 2014
Biblia ya Sauti: Biblia Habari Njema