Posted on 2021-03-312021-06-08 by Mipango ya usomaji – Machi 2021 MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama Mkristo Siku 5 Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema! Mwongozo wa KiMungu Siku 7 Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na Mchungaji Kiongozi, Craig Groeschel, anakutia moyo na kanuni saba kutoka kwenye kitabu chake cha Mwongozo wa Kimungu ili kukusaidia kupata busara ya Mungu kwa maamuzi yako kila siku. Gundua mwongozo wa kiroho unaohitaji ili kuishi hadithi ya maisha ya kumheshimu Mungu utakayopenda kuhadithia. Vitendo vya Toba Siku 5 Toba ni moja ya hatua muhimu sote huchukua tunapokuja kumjua Yesu kristo kama mwongozi wa maisha yetu. Toba ni kitendo chetu na msamaha ni majibu ya Mungu kwetu kutokana na mapenzi yake kamili kwa ajili yetu. Ndani ya siku tano na kupitia masomo haya, utapokea somo la biblia kila siku na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kuelewa vyema umuhimu wa toba katika kutembea kwetu na Kristo.