Posted on 2019-11-012021-10-01 by Mipango ya usomaji – Novemba 2019 Zaburi siku 31 Usomaji wa kitabu cha Zaburi niya muhimu kwa kila muda ya haja. Wakati unapitia wakati mgumu, kitabu cha Zaburi kinaweza kua kama faraja na kuweka moyo. Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika Bwana siku 30 Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa “My Utmost for His Highest”, katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu. Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku – Hekima siku 5 Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, “Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako.”Biblia inasema, “Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.” Zaburi 119:2 (BHN) Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila Siku siku 7 Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog.