Posted on 2020-03-012021-10-11 by Mipango ya usomaji – Machi 2020 Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamoja siku 7 Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pamoja katika mpango huu wa Biblia wa siku 7 kwa pamoja, mafunzo ya vijana kutoka Life. Church. Safari ya Agano Jipya kwa Siku 60 siku 60 Mpango huu wa kusoma Biblia utawaongoza kupitia Agano Jipya katika siku 60. Vitabu vingi vitawajulisha, lakini Biblia ina uwezo wa kukugeuza. Soma tu uchaguzi wa kila siku na utastaajabishwa na uwezo, ufahamu na mabadiliko ambayo yatatokea katika maisha yako. Marko siku 8 Mangu huu rahisi utakuongoza ndani ya kitabu cha Injili iliyo andikwa na Marko kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kutaka siku 7 Katika siku hizi 7 za kusoma na kujifunza, Beth Moore anatumia maswali kutoka katika Maandiko Matakatifu ili kukuongoza kwenye uhusiano wa ndani zaidi na Yeye anayekujua vizuri. Alama za uandishi zilizopotoka mwisho wa sentensi zinaonyesha udadisi, hamu au labda wasiwasi. Swali ni mwaliko toka katika hali hatarishi hadi ukaribu wa ndani zaidi. Biblia haiachi ukaribisho huo. Mara kwa mara tunaona watu wa Mungu wakimuuliza Muumbaji wao maswali. Na pia tunamwona Mungu Muumbaji akiuliza maswali kwa viumbe wake. Changamoto ni kupokea mwaliko. Jifunze kuchimba ndani ya Neno la Mungu, kujibu maswali ya Mungu, na kuleta maswali mbele Zake. Ruhusu alama za uandishi zilizopotoka ziwe ramani ya kusogeza uhusiano wako na Baba yako kuwa wa ukaribu zaidi.