Posted on 2020-05-012021-10-11 by Mipango ya usomaji – Mei 2020 Hujaachwa: Kupata uhuru kama watoto wa Baba halisi siku 5 Louie Giglio, Mchungaji na Mwanzilishi wa Passion Movement, anashiriki nasi mpango huu wa siku 5 kuelewa sifa za Mungu katika kubadili maisha – kama baba kamili anayetaka utembee katika uhuru kama mtoto wake. Mpango wa Mungu katika maisha yako siku 6 Je, nini mpango wa Mungu juu ya maisha yako? Ni maswali ya kawaida tuliyonayo wote kama wafuasi wa Kristo. Ila kama tukiwa waaminifu, wazo la mpango wa Mungu katika maisha yetu linaweza kuwa gumu kwetu. Katika siku hizi 6 za mpango wa kujisomea Biblia, tutajifunza jinsi mpango wa Mungu usivyo mgumu kama tunavyoweza kufikiri, ila ni mwema kuliko tunavyoweza kufikiria Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu Uzazi siku 7 Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion – wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni za neno la Mungu katika eneo hili muhimu katika maisha yao. Kila siku ya ibada hii inajumuisha taswira ya mstari unaoweza kuutumia kukusaidia kushirikia safari yako mwenyewe. Warumi siku 8 Mpango huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Waroma na niya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.