Posted on 2020-08-012021-10-11 by Mipango ya usomaji – Agosti 2020 Kutafuta Amani siku 10 Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu–Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo. Kutafuta Karoti siku 7 Wote tunatafuta kitu. Mara nyingi ni kitu ambacho hakipatikani–kazi nzuri, nyumba bora zaidi, familia bora, kukubalika na wengine. Lakini hii haichoshi? Je, kuna njia bora zaidi? Pata katika mpango wa new Life.Church Bible, ikifuatana na mfululizo wa ujumbe wa Mchungaji Craig Groeschel’s, Kutafuta Karoti. Tumaini, Jibidishe, Na Pumzika siku 4 Biblia inatuagiza kufanya kazi kwa bidii, lakini pia inatuambia ni Mungu– siyo sisi –anayetoa matunda ya kazi yetu. Kama mpango huu wa siku nne utakavyoonesha, taaluma ya kikristo lazima ikubali mvutano kati ya “kuamini” na “kujibidisha” ili kupata mapumziko halisi ya Sabato. Waefeso siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Waefeso na ni cha maana kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.