Posted on 2021-04-012021-10-15 by Mipango ya usomaji – Aprili 2021 Maombi ya Yesu siku 5 Tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika uhusiano, na uhusiano wetu na Mungu sio tofauti. Mungu anataka tuwasiliane naye kwa maombi—Kitu ambacho hata mwanawe, Yesu Kristo alifanya. Katika mpango huu, utajifunza kutoka kwa mfano wa Yesu, na utapewa changamoto ya kutoka katika shughuli nyingi za maisha na ujionee nguvu na mwongozo maombi hutoa. Yohana siku 10 Mpango huu rahisi utakuongoza kupitia njia ya Injili kulingana na Yohana kuanzia mwanzo hadi mwisho Tusome Biblia Pamoja (Aprili) siku 30 Sehemu ya 4 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia nzima pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya kazi vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na Agano la Kale, na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya 4 inajumuisha vitabu vya Mathayo na Yakubu. Maombi Hatari siku 7 Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, “Dangerous Prayers” yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.