Posted on 2021-06-302021-07-05 by Mipango ya usomaji – Juni 2021 Maombi Hatari Siku 7 Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, “Dangerous Prayers” yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini. Kutafuta Njia ya Kumrudia Mungu Siku 5 Je, unatafuta mengi kutoka kwa maisha? Kutaka mengi ni kuwa na hamu ya kumrudia Mungu— popote uhusiano wako na Mungu upo sasa. Sisi sote hushuhudia ishara—au muamko—tunapotafuta kumrudia Mungu. Safari kupitia kwa moja wepo ya miamko hizi na kupunguza umbali kati ya ulipo sasa na wapi unataka kuwa. Tunataka kumpata Mungu, anataka hata mengi yapatikane.. Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi! Siku 7 Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt Maombi ya Yesu Siku 5 Tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika uhusiano, na uhusiano wetu na Mungu sio tofauti. Mungu anataka tuwasiliane naye kwa maombi—Kitu ambacho hata mwanawe, Yesu Kristo alifanya. Katika mpango huu, utajifunza kutoka kwa mfano wa Yesu, na utapewa changamoto ya kutoka katika shughuli nyingi za maisha na ujionee nguvu na mwongozo maombi hutoa. Kutafuta Amani Siku 10 Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu–Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo. Kuua Nguvu zinazoangamiza na John Bevere Siku 7 Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung’oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka. 1 & 2 Timotheo Siku 5 Mpango huu ita kuchukua ndani ya 1 & 2 Timotheo na itakua vizuri kwa usomaji wa upekee ama ya kundi. Kubarikiwa Siku 7 Unaishi vipi maisha yaliyo barikiwa? Naamini kila mtu anahamu na anatafuta jibu hili. Miongoni mwa wahusika mbalimbali katika Biblia, kuna mmoja hasa ambaye napenda. Jina lake halijatajwa, lakini anaishi kwa kanuni za Biblia. Huyu shujaa wangu wa Kibiblia ndiye mtu mwema aliyetajwa katika Zaburi 112.