Posted on 2021-10-012021-09-22 by Mipango ya usomaji – Oktoba 2021 Yakobo Siku 3 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Yakobo na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja ( Octoba) Siku 31 Sehemu ya 10 kati ya mfululizo wenye sehemu 12 katika mpango huu unaziongoza jamii kuipitia Biblia nzima katika siku 365. Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 10 inavihusisha vitabu vya Mhubiri, Yona, Yeremia na Maombolezi Kuamini Mungu ni vyema Bila kujali lolote Siku 5 Kuna jumbe fulani siku hizi, nje na ndani ya Kanisa, ambazo zimepaka tope ujumbe wa kweli wa fadhili za Mungu. Ukweli ni kwamba, Mungu hashurutishwi kutupea vitu vizuri—lakini anataka! Siku tano zijazo zitakusaidia kuangalia upya kando yako kwa macho yanayoona vitu vinavyokupotosha kila siku na kuona wema chungu nzima wa Mungu.