Posted on 2021-11-012021-10-28 by Mipango ya usomaji – Novemba 2021 1 & 2 Petro siku 4 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha 1 & 2 Petro na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Tuisome Biblia Pamoja (November) siku 30 Sehemu 11 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unazielekeza jamii kupitia Biblia nzima katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 11 inajumuisha vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Ezekieli, Hosea na Ufunuo wa Yohana. Vitendo vya Toba siku 5 Toba ni moja ya hatua muhimu sote huchukua tunapokuja kumjua Yesu kristo kama mwongozi wa maisha yetu. Toba ni kitendo chetu na msamaha ni majibu ya Mungu kwetu kutokana na mapenzi yake kamili kwa ajili yetu. Ndani ya siku tano na kupitia masomo haya, utapokea somo la biblia kila siku na ibada fupi iliyoundwa kukusaidia kuelewa vyema umuhimu wa toba katika kutembea kwetu na Kristo.