Posted on 2022-01-02 by Mipango ya usomaji – Januari 2022 Tusome Biblia Pamoja (Januari) siku 31 Sehemu ya kwanza ya msururu wa sehemu 12, mpango huu huongoza jamii kupitia Biblia yote pamoja kwa siku 365. Waalike wengine kujiunga kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na la Kale, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote kote. Sehemu ya kwanza inajumuisha vitabu vya Luka, Matendo, Danieli na Mwanzo. Yohana siku 10 Mpango huu rahisi utakuongoza kupitia njia ya Injili kulingana na Yohana kuanzia mwanzo hadi mwisho Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika Bwana siku 30 Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa “My Utmost for His Highest”, katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.