Posted on 2022-04-02 by Mipango ya usomaji – Aprili 2022 Tusome Biblia Pamoja (Aprili) siku 30 Sehemu ya 4 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia nzima pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya kazi vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na Agano la Kale, na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya 4 inajumuisha vitabu vya Mathayo na Yakubu. Matendo siku 14 Mpango huu rahisi utakuruhusu kujifunza kuhusu Mitume na kanisa la mwanzo. Ingia katika Kusudi siku 5 Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii.