Posted on 2022-06-02 by Mipango ya usomaji – Juni 2022 Tusome Biblia Pamoja (Juni) siku 30 Sehemu ya 6 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu huongoza jamii kupitia Biblia yote pamoja kwa siku 365. Waalike wengine kujiunga kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikilizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na la Kale, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote kote. Sehemu ya 6 inajumuisha vitabu vya Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, Yonah, Waamuzi, Ruthu na Samweli wa kwanza. Siku Sita Za Majina Ya Mungu siku 6 Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God’s Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017. Ufunuo siku 11 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Ufunuo na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi.