Posted on 2023-04-28Mipango ya usomaji – Mei 2023 Kugeuka na Kurudi Upande wa Pili Kutoka Uraibu siku 3 Ikiwa maisha yako hayako katika mpangilio na Neno la Mungu, hakika utapatwa na matokeo machungu. Wengi wamepambana na afya yao, kupoteza ajira, na mahusiano, na kujipata kwamba wanahisi kwamba wapo mbali na Mungu kwa sababu ya uraibu. Inaweza kuwa uraibu wenye uzito kama vile mihadarati au ponografia ama uraibu ndogo, kama chakula ama burudani, uraibu unavuruga maisha yetu. Mruhusu mwandishi mashuhuri Tony Evans akuonyesha njia ya uhuru. Mbona Mungu ananipenda? siku 5 Maswali: Ikija kwa Mungu, tuna maswali mengi sana. Kwa sababu ya tamaduni zetu, swali moja ambalo tutajipata tukijiuliza ni, “Mbona Mungu ananipenda?” au “Ni vipi atanipenda?” Mpango huu unashirikisha jumla ya vifungu 26 vya Biblia—Kila kifungu kikiongea juu ya upendo wa Mungu usiokuwa na shaka.
Posted on 2023-03-30Mipango ya usomaji – Aprili 2023 Kwa nini Pasaka? siku 5 Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke kujua haya? Katika mpango huu wa siku tano, Nicky Gumbel anatoa majibu ya kuvutia kwa maswali hayo. 1 & 2 Timotheo siku 5 Mpango huu ita kuchukua ndani ya 1 & 2 Timotheo na itakua vizuri kwa usomaji wa upekee ama ya kundi.
Posted on 2023-03-02Mipango ya usomaji – Machi 2023 Siku Sita Za Majina Ya Mungu siku 6 Kutoka kwenye majina mengi ya Mungu, ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili. Zaidi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonesha zaidi ya majina 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake kumsaidia mwamini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Dondoo kutoka Experience the Power of God’s Names: A Life-Giving Devotional , ya Dr. Tony Evans. Eugene, OR: Harvest House Publishers, 2017. Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila Siku siku 7 Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjilisti Matt Brown ametayarisha mpango huu wa masomo ambayo yanapatikana katika kitabu chake cha masomo ya siku 30 kilichoandikwa na Matt Brown na Ryan Skoog. Ipe Kazi Yako Maana siku 4 Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. Kuishi kwa Roho: Ibada Pamoja na John Piper siku 7 Masomo 7 ya Ibada kutoka kwa John Piper kuhusu Roho Mtakatifu
Posted on 2023-02-02Mipango ya usomaji – Februari 2023 Yesu Ananipenda siku 7 Ikiwa mtu angekuuliza, “Ninahitaji kuamini ipi ili niwe Mkristo?” ungemjibu vipi? Kwa kutumia maneno ya wimbo upendwao, “Yesu anipenda, kweli ninajua, kwani Biblia inasema”, mhubiri aliyekuwa mwanahabari anakusaidia kuelewa unachoamini na sababu. Mwandishi maarufu John S. Dickerson anafafanua imani za kimsingi za Kikristo kwa uwazi na uaminifu na kuashiria mbona imani hizi ni muhimu. Ingia katika Kusudi siku 5 Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii. Muda wa kupumua siku 5 Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa… Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumua. Mungu anakupa fursa ya kubadilishana maisha yako yenye haraka na amani yake. Mpango huu utakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo. Kukombolewa kwa ndoto siku 7 Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.
Posted on 2023-01-02Mipango ya usomaji – Januari 2023 Mwaka Mpya, Rehema Mpya siku 15 Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku. Neno Moja Litakalobadilisha Maisha Yako siku 4 NENO MOJA husaidia kurahisisha maisha yako kwa kulenga tu NENO MOJA kwa mwaka mzima. Urahisishaji wa kugundua neno ambalo Mungu amekuwekea inafanya kuwa kichochezi cha maisha yako kubadilika. Vurugu na utata husababisha kuchelewesha na kulemaza, ilhali urahisishaji na lengo husababisha mafanikio na uwazi. Ibada hii ya siku nne inakuonyesha jinsi ya kupata kiini cha nia yako kwa maono ya neno moja kwa mwaka.