Posted on 2024-08-01Mipango ya usomaji – Agosti 2024 Kukua katika Upendo siku 5 Kinachojalisha kwa kweli ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine, lakini tunawapendaje kwa ufanisi? Ukweli ni kwamba, hatuwezi kuwapenda watu vizuri kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini tunapomuangalia Mungu na kunyenyekea, tunaweza kuishi katika nguvu kamili ya upendo wa Mungu. Jifunze zaidi kuhusu kukua katika upendo katika mpango wa siku 5 kutoka wa Mchungaji Amy Groeschel. Tusome Biblia Pamoja (Agosti) siku 31 Sehemu ya 8 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia nzima pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikizi—sikiliza chini ya dakika 20 kila siku. Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na Agano la Kale, na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya 8 inajumuisha kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Kwanza na ya Pili, Wathesalonike wa kwanza na Pili na Ezra.
Posted on 2023-12-01Mipango ya usomaji – Desemba 2023 Luka siku 12 Mpango huu rahisi utakuongoza ndani ya kitabu cha Injili iliyo andikwa na Marko kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Tusome Biblia Pamoja ( Desemba) siku 31 Sehemu ya 12 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unaziongoza jamii kupitia Biblia youte pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 12 inavijumuisha vitabu vya Isaya, Mika, Petro wa Kwanza, Petro wa Pili, Yohana wa Kwanza, Yohana wa Pili, Yohana wa Tatu, Yohana na Yuda
Posted on 2023-11-01Mipango ya usomaji – Novemba 2023 Tuisome Biblia Pamoja (November) siku 30 Sehemu 11 katika mfululizo wenye sehemu 12, mpango huu unazielekeza jamii kupitia Biblia nzima katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 11 inajumuisha vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Ezekieli, Hosea na Ufunuo wa Yohana. Wagalatia siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Wagalatia na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.
Posted on 2023-09-02Mipango ya usomaji – Septemba 2023 Tusome Biblia Pamoja (Septemba) siku 30 Sehemu ya 9 kati ya 12 kwenye mpangilio unaoongoza jamii kusoma Biblia nzima pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 9 inajuisha vitabu vya Nehemia, Esta, Timotheo wa kwanza na wa pili, Yoeli, Amosi, Obadia, Nahumu, Habakuki, Sefania, Tito, Philomeno, Yakobo, Hagai Zekarai na Malaki
Posted on 2023-06-25Mipango ya usomaji – Julai 2023 Ngumu na Lisa Bevere siku 6 Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura. Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku – Hekima siku 5 Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, “Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako.”Biblia inasema, “Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.” Zaburi 119:2 (BHN) Adui wa Moyo siku 5 Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adui wanne wa moyo — hatia, hasira, tamaa, na wivu — na kukufunza jinsi ya kuwaondoa.