Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya

Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya

1  
Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.

2  
Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka.

3  
Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.

4  
Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako.

5  
Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.

6  
Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri.

7  
Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.

8  
Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.

9  
Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.

10  
Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.

11  
Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.

Psalm 37 in Swahili

Psalm 37 in English

CategoriesIsio-gawanyo