Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali

Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali

2  
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali

3  
mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

4  
Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

5  
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

6  
Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7  
Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8  
Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

9  
Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa

10  
bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.

11  
Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

12  
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

James 1 in Swahili

James 1 in English

CategoriesIsio-gawanyo