Posted on 2020-06-012021-10-11 by Mipango ya usomaji – Juni 2020 1 Wakorintho siku 8 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha 1 Wakorintho na itakua ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Hekima Kamilifu: Safari ya Siku 7 ya akina Baba siku 7 Inashangaza kiasi ambacho baba zetu wanatufinyanga. Hakuna mtu anayeepuka nguvu na mvuto wa baba yao wa kidunia. Na kwa sababu wanaume wengi wanahisi kuwa hawako tayari kuwa baba, ni muhimu kutafuta mwongozo – kwenye Maandiko na kutoka kwa baba wengine. Hekima Kamilifu ni safari kuelekea hekima na busara kwa kina baba, inayohusisha kanuni na hekima kutoka kwenye Maandiko pamoja na uzoefu wa baba mwenye umri mkubwa na hekima zaidi ambaye amejifunza kutokana na makosa yake. Ngumu na Lisa Bevere siku 6 Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya moyo wako—kukupa mwelekeo katika ulimwengu unaozurura.