Posted on 2020-07-012021-10-11 by Mipango ya usomaji – Julai 2020 Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha Yako siku 5 Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi. Kuweka Muda Wa Kupumzika siku 5 Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu. Mambo yote ni mapya siku 5 Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jinsi mwenendo wa wakristo unaweza kuonekana unapingana na tabia zetu za asili, lakini inathibitisha kwamba wa milele na bora zaidi kwa nje. Katika siku tano hizi za mpango huu wa masomo, utavumbua vitu kama: jinsi ya kushughulika na mahusiano magumu, kumwamini Mungu na heshima yako, ukisimamisha utambulisho wako katika Kristo, kuelewa kusudi la mateso na upaji wa Mungu ndani yake, na jinsi tunavyotakiwa kuwa nuru ya injili ulimwenguni. Wagalatia siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Wagalatia na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi.