Posted on 2020-09-012021-10-11 by Mipango ya usomaji – Septemba 2020 Ipe Kazi Yako Maana siku 4 Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. Hatua Sita Ya Uongozi Bora Zaidi siku 7 U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua. Adui wa Moyo siku 5 Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adui wanne wa moyo — hatia, hasira, tamaa, na wivu — na kukufunza jinsi ya kuwaondoa. Kuua Nguvu zinazoangamiza na John Bevere siku 7 Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung’oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka.