Posted on 2021-03-012021-10-15 by Mipango ya usomaji – Machi 2021 Kutafuta Amani siku 10 Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu–Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo. Kufuata Amani siku 7 Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano yako na wengine na uombee dunia tunayoishi. Somo hili linatumia hekima kutoka methali za Afrika kutusaidia kufunua amani ya kweli ya Mungu. Amani ya Mungu siku 4 Neno la Mungu linatuambia kwamba Hutoa amani ” ipitayo ufahamu wote” (Wafilipi 4:7 SUV). Katika mafundisho haya ya siku nne, wewe na watoto wako muamgalie kwa makini maeneo katika maisha yetu tunapoweza kupata amani hiyo. Kila siku inajumuisha hitaji la maombi, kusoma maandiko kidogo na ufafanuzi, mazoezi ya kufanya, na maswali ya kujadili. Oswald Chambers: Amani – Maisha kwenye Roho siku 30 Amani: Maisha ya Roho ni hazina ya msukumo ya nukuu kutoka kwenye kazi za Oswald Chambers, mwandishi mpendwa ulimwenguni wa ibada na mwandishi wa My Utmost for His Highest. Pata mapumziko kwa Mungu na pata uelewa zaidi wa umuhimu wa amani ya Mungu kwenye maisha yako. Waebrania wiki 1 Mpango rahisi kama huu utakupeleka ndani ya kitabu cha Waebrania na itakua vizuri kwa funzo ya upekee ama ya kundi. Tumaini Linaloishi: Hesabu kuelekea Pasaka siku 3 Giza linapokuzunguka, ulikabili namna gani? Kwa siku 3 zijazo, zama katika hadithi ya Pasaka na ugundue jinsi ya kushikilia tumaini pale unapojisikia kuachwa, mpweke au usiye wa thamani.