Posted on 2021-07-102021-07-26 by Mipango ya usomaji – Julai 2021 1 Wakorintho Siku 8 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha 1 Wakorintho na itakua ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Julai) Siku 31 Sehemu ya 7 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia yote pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge nawe kila wakati unapoaza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikizi—sikiliza kwa chini ya dakika 20 kila siku! Kila sehemu inajumuisha sura za Agano la Kale na Agano Jipya, pamoja na Zaburi ikiwa imetawanyika kote kote. Sehemu ya saba inajumuisha vitabu vya Samueli wa Pili, Wafalme wa Kwanza na wa Pili na Mariko. Mbona Mungu ananipenda? Siku 5 Maswali: Ikija kwa Mungu, tuna maswali mengi sana. Kwa sababu ya tamaduni zetu, swali moja ambalo tutajipata tukijiuliza ni, “Mbona Mungu ananipenda?” au “Ni vipi atanipenda?” Mpango huu unashirikisha jumla ya vifungu 26 vya Biblia—Kila kifungu kikiongea juu ya upendo wa Mungu usiokuwa na shaka. Kuweka Muda Wa Kupumzika siku 5 Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu.