Posted on 2021-08-05 by Mipango ya usomaji – Agosti 2021 Waefeso Siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Waefeso na ni cha maana kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Agosti) Siku 31 Sehemu ya 8 ya msururu wa sehemu 12, mpango huu unaongoza jamii kupitia Biblia nzima pamoja kwa siku 365. Waalike wengine wajiunge kila wakati unapoanza sehemu mpya kila mwezi. Msururu huu hufanya vyema na Biblia sikizi—sikiliza chini ya dakika 20 kila siku. Kila sehemu inajumuisha sura za Agano Jipya na Agano la Kale, na Zaburi ikiwa imetawanyika kote. Sehemu ya 8 inajumuisha kitabu cha Mambo ya Nyakati ya Kwanza na ya Pili, Wathesalonike wa kwanza na Pili na Ezra. Mazungumzo na Mungu Siku 12 Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote – mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda! Mpango wa kupigana Vita vya Kiroho Siku 5 Kwa haya mafundisho ya nguvu utaelewa kwa kina kuhusu jinsi ya kutengeneza njia ya kumpita adui na kuzuia mpango wake wa kuharibu maisha yako