Posted on 2021-09-052021-09-20 by Mipango ya usomaji – Septemba 2021 Wagalatia Siku 3 Mpango huu rahisi utakuchukua ndani ya kitabu cha Wagalatia na ni ya muhimu kwa mafundisho ya upekee ama ya kundi. Tusome Biblia Pamoja (Septemba) Siku 30 Sehemu ya 9 kati ya 12 kwenye mpangilio unaoongoza jamii kusoma Biblia nzima pamoja katika siku 365 Wakaribishe wengine kujumuika nawe kila mara unapoanza sehumu mpya kila mwezi. Mfululizo huu unaendana vyema na Biblia ya kusikiliza – sikiza kwa chini ya dakika 20 kwa siku. Kila sehemu inajumuisha sura kutoka agano la kale na agano jipya, pamoja na mgawanyiko wa Zaburi Sehemu ya 9 inajuisha vitabu vya Nehemia, Esta, Timotheo wa kwanza na wa pili, Yoeli, Amosi, Obadia, Nahumu, Habakuki, Sefania, Tito, Philomeno, Yakobo, Hagai Zekarai na Malaki Kutumia muda wako kwa ajili ya Mungu Siku 4 Ibada ya siku nne kutoka kwa R.C. Sproul, jinsi ya kutumia wakati wako kwa ajili ya Mungu. Kila Ibada inakuhimiza kuishi katika uwepo wa Mungu, chini ya mamlaka ya Mungu, kwa utukufu wa Mungu.