Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?

Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?

10  
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.

11  
Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.

12  
Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.

13  
Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.

14  
Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.

15  
Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.

16  
Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

17  
Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.

18  
Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.

19  
Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.

20  
Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.

21  
Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.

22  
Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.

23  
Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.

24  
Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.

25  
Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.

26  
Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.

27  
Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

28  
Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema

29  
Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.

30  
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.

31  
Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.

Proverbs 31 in Swahili

Proverbs 31 in English

Gundua: Kipengele Kipya Kabisa

Gundua

Kujulisha: Gundua

Wakati mwingine unaposoma au kusikiliza mistari fulani ya Biblia, inakuongoza katika maswali: Hii ina maana gani? Ni nani aliandika hii, na kwa nini? Ninawezaje kubaini vipi neno hili kwa maisha yangu?

Kipengele chetu kipya cha Kugundua kinaweza kusaidia!

Bonyeza tu iconi mpya ya Gundua wakati wowote unapoiona katika Usomi wa Biblia (Gundua), na utaona maudhui ya ziada ambayo itakusaidia kulijua Neno la Mungu kwa njia tofauti. Gundua inapatikana sasa, na video kutoka kwa washirika wetu LUMO!

Jaribu Kugundua leo, na ufaidike zaidi kutokana na muda wako katika Neno la Mungu.

Mungu ameuweka uhai katika maandiko yote. Ni muhimu kwa kutufundisha ukweli… kuyafanya maisha yetu mazima tena… muhimu kwa kutufundisha kufanya haki.

2 Timotheo 3:16

Ipate Sasa

Mipango ya usomaji – Mei 2019

App ya Biblia ya Watoto sasa inalinganisha vyombo vyote!

Maelezo kayika App ya Biblia ya Watoto

“Hey! Nyota zangu zote ziko!”

Mbele, tuzo za watoto wako zimehifadhiwa kwenye chombo ambapo walizopata. Ikiwa walipata chombo mpya, ao ikiwa uliwaruhusia kutumia App ya Biblia ya Watoto kwenye simu ingine, walipaswa kuanza upya mwanzo. Sivyo tena.

Sasa maendeleo imehifadhiwa kwa kila mmoja wa watoto wako, imeunganishwa kwenye vyombo vyako vyote!

Kama mzazi au mlezi, usasisha wa sasa wa App ya Biblia ya Watoto inakuwezesha kuingia kwa kutumia daftari ya YouVersion ilipo yako na kuanzisha avatari kipekee kwa kila mtoto. Kuongeza maelezo ni haraka na rahisi. Watoto wako wanaweza hata kuchagua avatari na rangi zao.

Pata App ilisasaishwa

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

7  
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa

8  
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

9  
Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?

10  
Au akiomba samaki, atampa nyoka?

11  
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?

12  
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Matthew 7 in Swahili

Matthew 7 in English