Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki

Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki

1  
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2  
Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3  
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

4  
Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5  
Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6  
Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.

Psalm 1 in Swahili

Psalm 1 in English

CategoriesIsio-gawanyo